Recent-Post

Hamisa, Zari na Wema uso kwa uso Nigeria


 Wanawake maarufu Hamisa Mobetto ,  Wema Sepetu pamoja na Zarina Hassan ‘Zari’ wanatarajia kuchuana katika tuzo za Africa Choice

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Oktoba 2021 nchini Nigeria ikiwa ni mara ya  21 tangu kuanzishwa ambapo jumla ya vipengele 32 kuwaniwa.

Hamisa na Zari ambao ni wazazi wenza wa nyota wa msanii  Diamond Platnumz, wanawania kipengele kimoja cha mabalozi wa bidhaa wenye mvuto.

Pia mrembo Wema Sepetu anawania kipengele cha mwigizaji bora wa kike akichuana na waigizaji kutoka nchi nyingine wakiwamo Zynnellzuh (Ghana), Pearlthusi (South Africa), Lindaosifo (Nigeria),Hlubimboya1 (South Africa),Nomzamom (South Africa) na Lillyafe (Nigeria).

Wengine waliotajwa kutoka Tanzania ni msanii   Idris Sultan (mchekeshaji bora), Irene Uwoya na Ben Breaker (Chaguo la watazamaji), Diamond Platnumz (Msanii wa mwaka),Millard Ayo (mtu mwenye mvuto),  Gabo Zigamba (mwigizaji wa kiume wa mwaka), Luluz Hair (muuza bidhaa za nywele wa mwaka).


Post a Comment

0 Comments