BoT YAWATAKA WAANDISHI KUWA SEHEMU YA KUVUTIA UWEKEZAJI KUPITIA KALAMU ZAO

 

Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo.

.............................................

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatamani wanahabari wawe sehemu ya kuvutia uwekezaji kupitia kalamu zao kwa kuandika habari zinazoibua fursa mbalimbali za kiuchumi, zinazopatikana nchini ili kuvutia wawekezaji na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kupitia fedha za kigeni.

Amesema habari zitakazoandikwa zikiainisha fursa mbalimbali zinazoonyesha fursa zinazopatikana katika kilimo cha Parachichi Nyanda za juu Kusini zitahamasisha wakulima wengi kujiingiza kwenye zao hilo na hatimaye kujikwamua kiuchumi na kuisaidia Taifa kupata fedha za kigeni.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya, Dk. Nicholaus Kessy kwa niaba ya Naibu Gavana wa (BoT) nchini, Bernard Kibesse wakati akifungua semina kwa Wahariri na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini inayofanyika katika tawi la (BoT) jijini Mbeya.

"Semina hii imejikita kuwafundisha wanahabari kuwa wabobezi wa habari za Uchumi, fedha na biashara kwa sababu wanahabari wakibobea katika eneo hilo wataweza kuandika kwa weledi habari zinazohusu sera mbalimbali za fedha pamoja na kuchambua kupitia vipindi, na makala zinazoeleza majukumu ya benki kuu Tanzania ,” amesema Dk. Kessy.

Ameongeza kuwa wanahabari wanapaswa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hususani Mikoa ya Nyanda za juu kusini ikiwamo vivutio vya uatlii na kilimo ili kuwavutia wawekezaji na watalii kutembelea Hifadhi za Taifa kama vile Kitulo, Ruaha, Katavi , Ziwa Ngosi na maeneo mengine yenye kuvutia.

Naye, Kaimu Meneja wa Mahusiano na Itifaki kutoka Benki ya Tanzania (BoT), Vicky Msina amesema semina inayotolewa kwa waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha inalenga kuwajengea uwezo kuchambua na kuandika habari kwa weledi zinazohusu majukumu ya benki.

Msina amesema miongoni mwa mambo wanayofundishwa wanahabari ni kutambua matumizi ya lugha za kifedha ili kuwasaidia wanahabari kuandika habari zitakazoeleweka kwa jamii.

“Hii ni semina ya tisa tangu kuanza kwa utaratibu huu, tumeona manufaa makubwa baada ya kuwapatia wanahabari mbalimbali nchini kuhusu masuala mbalimbali yanayofanywa na Benki kuu ya Tanzania pamoja na masuala mengine yanayohusu biashara na uchumi,” amesema Msina.
 
Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Mbeya akifungua semina ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini inayofanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya katikati ni Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo kushoto ni Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina na kulia ni Emmanuel Lengwa wa ITV na mtunza muda wa semina hiyo
 
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi.
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ili kumkaribisha mgeni rasmi kulia ni mgeni rasmi Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya akimsikiliza.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki (BoT) Bi. Vick Msina akitoa neno la utangulizi kabla ya mgeni rasmi kufungua semina hiyo kulia ni Dorcas Mtenga Mwenyekiti wa Semina na katikati ni Dk Nicholas Kessy Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania BoT.
Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakiwa na majukumu mbalimbali ili kufanikisha semina hiyo hapa wakijadiliana jambo.
  
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika seminahiyo inayofanyika kwenye tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mbeya.
 
Dorcas Mtenga Mwandishi mwandamizi wa Channel Ten na mwenyekiti wa semina hiyo akizungumza na washiriki wa semina hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa semina hiyo.
    

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments