Vijana wametakiwa Kujua na Kufata taratibu na Sheria Za
Barabarani Wakati Wa Kufanya Shughuli Mbali Mbali Za Usafilishaji Ilikuepuka Migogoro
Na Wanao Simamia Sheria Za Barabarani.
Kauli Hiyo Imesemwa Na Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana(UVCCM) Mkoa
Wa Kigoma Bi Geraidina Kabululu Wakiambatana Na Mbunge Viti Maalum Kundi La
Vijana Bi Silivia Sevula Wakati Wakiendelea Kupokea Changamoto Mbali Mbali Za Waendesha Bodaboda Mkaoni
Kigoma
Bi Kabululu Ameeleza Kuwa Changamoto Za Kukamatwa Kwa Boda Boda Wakiwa Katika Shughuli Zao Na Jeshi La Polisi Ni Tatizo Ambalo Linazungumzika na Tayari Wamekutana na pande Zote Mbili Ilikumaliza Tatizo Hilo Mkoani Kigoma.
Aidha Ziara Ya Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Mkoa Wa Kigoma Bi. Geraidina Kabululu Na Mbunge Kundi La VIjana Bi Silivia Sevula Ya Kusikiliza Changamoto Mbali Mbali za Vijana Imeendelea Katika Wilaya Kasulu,Buhigwe,Kibondo Na Kakonko Mkaoani Kigoma.
Vijana Wametakiwa Kuwa Mstari Wa Mbele Katika Kazi Mbali Mbali Za Jami Na Kujitolea Kwa Moyo Mmoja Kwani Vijana Ndio Uti Wa Mgongo Wa Taifa
0 Comments