KATIBU MKUU CCM AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA, AHIMIZA UTUNZWAJI WA MIUNDOMBINU

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani huku akitumia nafasi hiyo kutoa maelekezo na maagizo katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kuhakikisha wananchi wanatunza vyanzo vya maji pamoja na miundombinu.


Akizungumza leo na wananchi wa Kata ya Mwakitolyo mkoani Shinyanga, Chongolo amewapongeza wananchi hao kwa kuendelea kupata fedha kutoka serikalini kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji.

“Ndugu zangu nimekuja hapa, nimepata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa tanki la maji lililowekwa eneo ambalo wananchi watapata maji kwa asilimia 100.Hongereni na niwapongeze kwa kutunza eneo lile,

“Nitoe mwito katika maeneo mengine wahakikishe wanatenga maeneo kwa ajili ya uhifadhi kwani yanatija sana, sio kila eneo anatakiwa kwenda ng’ombe , sio kila eneo linatakiwa kuchimbwa, sio kila eneo linatakiwa kutumiwa kwa kila kitu lazima muhifadhi kwa ajili ya matumizi maalum ndani ya maeneo yenu”.

Akizungumza zaidi akiwa eneo hilo Chongolo amesema tanki la maji ambalo limejengwa eneo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi ujao lakini mtandao wa maji umewekwa na zaidi ya Sh.bilioni mbili zimetumika.“Kuna fedha nyingi zimeendelea kutolewa na Serikali kwa ajili ya kuweka mtandao wa maji.”

Hivyo amewaomba wananchi hao kuhakikisha wanatunza miundombinu ya maji kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.“Ndugu zangu wa Kijiji cha Mwakitorio niwaombe sana najua ninyi wengi hapa ni wachimbaji wa madini, sehemu yanakopita matanki haya pamoja na miundombinu yake msiende kuchimba na kuyakata mabomba.

“Lindeni miundombinu hii ya maji, fedha nyingi zimetumika.Uamuzi wa Rais Samia na Serikali anayoingoza kuamua kuweka miundombinu hiyo sio uamuzi mdogo , unahusisha fedha nyingi kwa lengo la kuhudumia wananchi,”amesema Chongolo na kufafanua idadi ya wananchi kwenye Kata hiyo wameendelea kuongeza siku hasi siku.

Amesisitiza miundombinu ya maji ni muhimu kwa kizazi cha sasa na kijacho, na kwamba wakichezea miundombinu ya maji hata kazi ya uchimbaji madini itakuwa ngumu huku akitumia nafasi hiyo kuipongeza mamlaka ya Maji Shinyanga kwa kazi nzuri na ametoa mwito kwa mamlaka hiyo kuendelea kusimamia vema miradi ya maji.

Ametoa rai kwa RUWASA kuendelea kutekeleza miradi ya maji ili wananchi wa maeneo yote ya vijijini wapate maji safi na salama kama ambavyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inavyotaka kuona inaongeza mtandao wa upatikanaji maji.

Kwa upande wake Mhandisi Patrick Nzamba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji Kashwasa amesema ujenzi wa tanki la maji Mwakitoryo unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga ambao unalenga kuhudumia wananchi zaidi ya 14000 na mradi huo unahusisha ujenzi wa tanki, ulazaji wa mabomba , ujenzi wa uzio na nyumba ya mlinzi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipanda ngazi za tanki la maji lenye uwezo wa kubeba lita laki 5 na kuhudumia wakazi 14600 wa kijiji cha Mwakitolyo ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya mradi wa ujenzi wa tanki la maji litakalo hudumia wakazi 14600 wa kijiji cha Mwakitolyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji KASHWASA Mhandisi Patrick Nzamba (kushoto) mara baada ya kukagua ujenzi wa tanki la maji Mwakitolyo unaogharimu zaidi ya shilingi za Kitanzania milioni 364,ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa Shina namba 9 Tawi la Mwakitolya Mzee Ali Matembele (kulia) alipowasili kusalimia na kuzungumza na wakati wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiwa ameongoza

na Mwenyekiti wa Shina namba 9 Tawi la Mwakitolyo Mzee Ali Matembele (njano) akiwemo Mbunge wa jimbo la Solwa Mhe Ahmed Ally Salum alipokwenda kusalimia na kuzungumza na wakazi wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga.

 









Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Katibu wa Shina namba 9 Tawi la Mwakitolya Ndugu Amos Yohana (kulia) alipowasili kusalimia na kuzungumza na wakati wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipandisha bendera ya Chama katika shina namba 9 kuashiria uzinduzi wa shina hilo, ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 mkoani Shinyanga

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments