DC MURO AINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI HEKARI 3,000 VIJIJI VYA ULYAMPITI NA MWAU WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry Muro pamoja na wataalamu wa ardhi kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri leo tarehe 29/07/2022 wamelazimika kukutana na baadhi ya wananchi wa vijiji vya ulyampiti kata ya UNYAHAATI na mwau kata ya Mang'onyi pamoja na baadhi ya wananchi waliowekeza kwenye shamba la pamoja la kilimo cha korosho lenye hekari elfu tatu

Dc Muro ambae amelazimika kutoa ufafanuzi wa Mgogoro wa mpaka wa vijiji hivyo na kusema kwa mujibu wa vipimo vya kitalaamu eneo lenye hekari elfu tatu liko kijiji cha ulyampiti na si vinginevyo

Dc Muro amewataka wananchi ambao waliomba kwa maandishi kupitia kijiji cha mwau kukaa kwenye maeneo hayo wasiondolewa na uongozi wa ulyampiti kwani changamoto imesababishwa na viongozi wa kijiji cha mwau kutokufuata utaratibu hivyo wananchi waliopewa kwa MAANDISHI maeneo hayo kubaki walipo na wasisumbuliwe

Hata hivyo Dc Muro amewataka wananchi waliovamia maeneo hayo na kuyatumia pasipo kuomba katika kijiji chochote wawe wameondoka ndani ya siku 30 kuanzia sasa na kuwapisha wananchi waliolipiwa maeneo hayo kwa ajili ya kilimo cha korosho ambapo tayari halmashauri ya kijiji cha ulyampiti wameshakusanya zaidi ya milioni 51 kutoka kwa wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo cha pamoja cha korosho

Akihitimisha mgogoro huo Dc Muro amesema kwa mwananchi yoyote anaetaka kuishi kwenye eneo hilo la mradi lazima aombe kwa maandishi na awe tayari kulipia gharama za kupewa ardhi na uongozi wa kijiji cha ulyampiti na si vinginevyo

Katika hatua nyingine Dc Muro amewaonya baadhi ya wananchi na viongozi kutoka kijiji cha mwau kuacha tabia ya kuvamia mashamba hayo na kuchoma moto mikorosho iliyopandwa na wananchi wanaowekeza katika eneo hilo na kusisitiza hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuchoma miti ya korosho inayopandwa.



                             
 Chanzo  Na Offisi Ya Mkuu Wa Wilaya Ikungi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments