VIDEO: Ladack Chasambi hapoi ameanza Mazoezi Mepesi Visiwani Zanzibar

Ladack Chasambi ameanza Mazoezi Mepesi yakujiweka Fiti kabla ya Mazoezi ya Jumla siku ya Kesho, Chasambi ametambulishwa Leo Kujiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Zaidi, Simba Sc imeendelea kuweka salama malengo yao ya kuchukua taji la pili msimu huu ikitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba kwa bao 1-0.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Simba Sc kuifuata Singida Fountain Gate ambao mapema jioni ilitangulia nusu fainali baada ya kuichapa Azam Fc kwa mabao 2-1.

Simba Sc haikuwa na dakika 90 rahisi mbele ya Jamhuri kama ambavyo ilikuwa ikidhaniwa kwani vijana hao wa Pemba walikuja na akili tofauti na mbinu na kuwabana vizuri wekundu hao kwa muda mwingi wa mchezo huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments