Diwani Kinyeto Azungumza na Wananchi wa Kibaoni – Atoa Shukrani na Kutangaza Mafanikio

                                         

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kibaoni, Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kindai, Omary Salum Kinyeto, ameendelea kuwasilisha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2020–2025. Akizungumza mbele ya wananchi, Diwani Kinyeto amesisitiza umuhimu wa vijana kutimiza vigezo ili waweze kunufaika na mikopo ya maendeleo, huku akibainisha kuwa wanawake wamepata zaidi ya milioni 56 kupitia mikopo ya vikundi.

Katika hatua nyingine, milioni 20 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida zimetumika kujenga maabara ya shule ya Sekondari ya Kindai, jambo linalolenga kuinua kiwango cha elimu ya sayansi kwa vijana wa kata hiyo.

Kwa upande wa huduma za kijamii, viti 135 vimenunuliwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za jamii, vikifanikishwa na ushirikiano kati ya Diwani na WODIS. Pia, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, kwa juhudi zake za kuendelea kuiombea miradi mkoani humo.

Mafanikio mengine ni pamoja na:

  • Barabara ya juu ya Munangi iliyogharimu zaidi ya Bilioni 1.9, iliyojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.
  • Kivuko cha chini (underpass) cha Kibaoni, ambacho kimeondoa hatari ya ajali kwa wakazi wa eneo hilo.
  • Zaidi ya Bilioni 3.1 zimetumika kwa miaka mitano kwenye miradi mbalimbali ndani ya Kata ya Kindai.

Diwani Omary Kinyeto ametoa pongezi kwa watendaji wa Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia Kata ya Kindai rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo. Pia, alieleza kuwa japo maabara moja tayari imepatikana, juhudi zinaendelea ili kupata nyingine kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri.

Mkutano wa tatu wa hadhara utafanyika siku ya Jumatatu katika mtaa wa dodoma Road na unatarajiwa kuendelea na mfululizo wa taarifa za utekelezaji wa ilani kwa wananchi wa kata hiyo.

Na hizi ni baadha ya picha katika mkutano huo.


                             
Na Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments