Bw. Kinyeto aliwasili katika Ofisi za Kata ya Kindai akiwa ameambatana na mke wake, Mwalimu Jasmini, pamoja na wanachama wa CCM na wapenzi wa chama hicho waliokuwa na hamasa kubwa ya kumshangilia.
Baada ya kuchukua fomu, Bw. Kinyeto aliwashukuru wananchi na wanachama wa CCM kwa kuendelea kumuunga mkono, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamo, amani na mashirikiano katika kata hiyo.
"Nawashukuru kwa imani hii kubwa mliyoionesha. Tutaendelea kushirikiana bega kwa bega kuimarisha maendeleo ya Kindai. Tuendelee kuilinda amani na kumwombea dua Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza vyema majukumu yake," alisema Bw. Kinyeto.
Aidha, aliwaasa wananchi wa Kindai kuhakikisha wanalinda miradi mbali mbali wa iliopo kata ya kindai kwa manufaa ya jamii, akiwataka kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na chama chao.
Kwa upande wake, mke wa diwani mteule, Mwalimu Jasmini, alitoa shukrani kwa wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, huku akiahidi kushirikiana nao katika kuunga mkono jitihada za maendeleo ya Kindai.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata ya Kindai, Bw. Hamisi Kitila, aliwashukuru wanachama na wananchi wote walioshiriki katika tukio hilo, akisisitiza mshikamano na mshirikiano katika kuendeleza kazi kubwa inayofanywa na CCM.
"Kazi yetu kubwa ni kuendelea kusema mazuri yanayofanywa na serikali yetu na chama chetu. Umoja wetu ndio ushindi wetu," alisema Kitila.
Tukio hilo limeacha hamasa kubwa kwa wananchi wa Kata ya Kindai ambao walionekana wazi kuonyesha mshikamo na mshikamano wa pamoja kwa CCM kuelekea uchaguzi Mkuu.
Na Bandola Media




0 Comments