RAIS WA WACHIMBAJI TANZANIA JOHNI BINA: “Mikopo Kwa Wachimbaji Itasaidia Kuchimba Kisasa na Kiteknolojia”

                                  

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Johni Bina, amesema serikali na taasisi za kifedha zimeendelea kuwaamini wachimbaji kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu ili kukuza sekta ya madini, hasa kwa wachimbaji wadogo wa Kitanzania. Amesema mikopo hiyo inalenga kuwawezesha wachimbaji kutumia teknolojia za kisasa zinazoongeza ufanisi na tija.

Bina ameongeza kuwa suluhu ya migogoro kwenye sekta ya madini inapatikana kupitia majadiliano ya amani na makubaliano mezani badala ya maandamano na migawanyiko.

Kauli hiyo ameitoa katika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan lililofanyika Shelui – Konkilangi, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, ambalo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na sekta ya madini.

                                       

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Antony Mavunde, alisema kuwa sekta ya madini kwa sasa inachangia kwa kiwango kikubwa mapato ya taifa kupitia makusanyo ya kodi na tozo, akibainisha kuwa madini ni miongoni mwa nguzo kuu za uchumi wa taifa.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Selemani Mwenda, alibainisha kuwa eneo la Konkilangi – Shelui ndilo eneo la kwanza kabisa Tanzania ambapo dhahabu ilianza kuchimbwa, na hivyo lina historia kubwa katika sekta ya madini nchini.

Kongamano hilo limewakutanisha wadau mbalimbali wa madini ambao wamempongeza Rais Samia kwa sera na mikakati inayokuza sekta ya madini, hususan kwa wachimbaji wadogo.

         
Abdul Ramadhani --Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments