Tanzia : JOB NDUGAI AFARIKI DUNIA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Spika Mstaafu na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Yustino Ndugai, kilichotokea leo tarehe 6 Agosti 2025 Jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ambaye amesema:

"Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo Jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Wenyeviti wa Mungano, na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. SpikaBunge limeeleza kuwa linaendelea kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya marehemu kuratibu mipango ya mazishi, huku taarifa zaidi zikiendelea kutolewa kadri maandalizi yanavyoendelea.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments