"Kiongozi wa Uhalisia, Anayeijua Singida Mjini" Yagi Kiaratu.

                                    

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa chaguo la wananchi kutokana na kuwapendekeza wagombea wenye weledi, uzoefu na uzalendo wa dhati kwa taifa. Katika Jimbo la Singida Mjini, jina la Mhe. Yagi Maulid Kiaratu limekuwa gumzo kubwa miongoni mwa wananchi, kutokana na historia yake ndefu ya uongozi na uwajibikaji.

Mhe. Yagi Kiaratu si jina jipya katika uongozi wa Singida. Kwa muda mrefu amehudumu kama Meya wa Manispaa ya Singida, nafasi iliyomwezesha kulifahamu kwa undani jimbo lote, kuanzia mitaa hadi kata zote za Singida Mjini. Uzoefu huu mkubwa unamwezesha kuelewa changamoto za wananchi wake na namna ya kushirikiana nao kuzitatua. Ni kiongozi ambaye hakika hafanyi maamuzi kwa nadharia pekee, bali anategemea uhalisia wa maisha ya wananchi wa kawaida.

Mbali na uongozi wa serikali za mitaa, Mhe. Yagi Kiaratu amejipambanua pia katika sekta ya michezo. Akiwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TTF), ameendelea kuonyesha namna michezo inavyoweza kuwa chombo cha mshikamano, ajira, afya na burudani kwa vijana na jamii kwa ujumla. Singida ni miongoni mwa miji inayozalisha vipaji vya michezo, na kwa nafasi hii, wananchi wa jimbo hili wanapata matumaini makubwa kwamba michezo itapewa kipaumbele maalum chini ya uongozi wake.

Mhe. Kiaratu ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi wa Singida Mjini pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha masuala ya msingi ya jamii yanapatiwa majibu ya kudumu. Ameweka msisitizo mkubwa katika kushirikisha wananchi kwa kila hatua, akiamini kuwa maendeleo ni matokeo ya mshirikiano wa viongozi na wananchi wao.

Kwa ujumla, Singida Mjini inakwenda kumpata mbunge mwenye maono, mwenye historia ya kutumikia wananchi wake, na mwenye upeo mpana wa kushirikiana na wadau kwa masilahi mapana ya jamii na taifa. Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuthibitisha kwa vitendo kwamba hakina upungufu wa viongozi bora, bali daima kimekuwa chimbuko la watu makini wenye weledi wa kusimamia maendeleo ya taifa letu.

Kwa Mhe. Yagi Kiaratu, wananchi wa Singida Mjini wanapaswa kuwa na matumaini makubwa ya kupata kiongozi asiye wa maneno, bali wa vitendo, mwenye uzoefu wa ndani na mapenzi ya kweli kwa watu wake. Huu ndio uthibitisho kwamba CCM bado ni nguzo thabiti ya maendeleo na mshikamano wa taifa letu.

Alufu Abdul Singida Mjini

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments