“Mlata: Kesho Njema ya Singida na Tanzania Ipo Mikononi mwa Mama Samia”

                                         

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mhe. Martha Mlata, amempokea kwa mapokezi ya shangwe na heshima kubwa, Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipowasili mkoani humo kuzungumza na wananchi.

Katika salamu zake, Mlata alimhakikishia Dkt. Samia kuwa Wanasingida wote wako imara nyuma yake, na kura zote za mkoa huo ni za mgombea urais huyo pamoja na wagombea wote wa CCM katika ngazi zote za uongozi.

“Tunayo kesho yenye baraka kubwa chini ya uongozi wa Dkt. Samia. Ni uongozi wenye tija kwa maendeleo ya Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla, kwani unajali maslahi mapana ya wananchi,” alisema Mlata.

Kwa upande wao, wagombea wa majimbo ya Wilaya ya Manyoni—Mhe. Pius Chaya (Manyoni Mashariki) na Mhe. Yohana Msita (Itigi)—wameendelea kuomba ridhaa ya wananchi huku wakiahidi kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030.

Akihutubia wananchi wa Manyoni, Dkt. Samia aliwapongeza kwa mshikamano wao na kueleza kuwa Manyoni kihistoria ni kitovu cha uelewa wa siasa za uhuru na maendeleo, kwani ndio eneo lililompokea Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza alipokuwa akiomba kura kupitia TANU.

“Wananchi wa Manyoni ni waelewa, na wameniunga mkono kwa dhati. Naamini Singida yote ni ngome ya CCM,” alisema Dkt. Samia.

Matukio Kwa Picha 



                                       


Na Abdul Bandola 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments