
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Samia Suluhu Hassan, amesema ujenzi wa mradi reli ya kisasa (SGR) ambayo itapita wilayani Manyoni kuelekea mkoani Tabora utaufungua Mkoa wa Singida na kutengeneza ajira nyingi za vijana.
Akizungumza na mamia ya wananchi mjini Manyoni baada ya kupokelewa akitokea Baki mkoani Dodoma, amesema katika utekelezaji wa mradi huo kutajengwa kituo ambapo kutakuwa na mambo ya biashara na uwekezaji na hivyo kufungua ajira kwa vijana.
Dk. Samia amesema kwa upande wa sekta ya elimu, wananchi wakiipa ridhaa CCM wamepaga Chuo cha Ufundi VETA ndani ya Wilaya ya Manyoni na kuongeza shule za msingi na sekondari katika maeneo ambayo yataainishwa.
“Oktoba 2024 nilifanya ziara na niliweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mkiwa-Itigi, ujenzi umefikia hatua nzuri.Tumeshampata mkandarasi pia tuliwahidi kuwa tutajenga barabara hii hadi Makongorosi mkoani Mbeya ili kuchochea biashara katia mkoa wa Singid ana Mbeya,” amesema.
Dk.Samia amesema mradi mwingine ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Manyoni ni ujenzi wa daraja la Sanza ambapo mkandarasi ameshapatikana na sasa zinatafutwa pesa ili ujenzi huo uweze kuanza mara moja.
Aidha, amesema kutajenga kituo cha kurusha matangazocha redio masafa ya FM katika mji wa Itigi ili TBC iweze kusikika vizuri na wananchi wa Manyoni waweze kupata fursa ya kusikiliza taarifa mbalimbali za nchi yao.
“Ndugu zangu niwahakikishia mambo mengine ya umeme kama kuna vitongoji ambavyo havijafikiwa na umeme, umeme tunakwenda kusambaza Tanzania yote lakini pia elimu ,maji safi na salama lengo ni kuhakikisha kila mtanzania apate maji safi na salama,” amesema Dk.Samia.
Kuhusu maji, amesema mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka mkoani Dodoma ambao utapitia Singida utauwezesha wananchi wa Mkoa wa Singida nao kuweza kupata maji safi na salama kutoka ziwa Victoria.
Aidha, mgombea huyo wa urais kupitia CCM Dk. Samia amesema katika kipindi cha ndani ya siku 100 wananchi watakapoipa ridhaa CCM atahakikisha Bima ya Afya inafanyika kwa majaribi




0 Comments