Hali ya kisiasa mkoani Singida imeendelea kuchukua sura ya kipekee baada ya mapokezi makubwa na yenye shamrashamra kumpokea Katibu wa Wazazi Taifa, Ally Hapi, aliyewasili kwa ajili ya kuendeleza mikakati ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Wananchi wa Singida, vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume, walijitokeza kwa wingi kumlaki Hapi kwa furaha kubwa, wakipaza sauti za hamasa na kuonyesha ishara ya mshikamano usiotetereka na CCM.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mlata, aliongoza shangwe hizo kwa uthabiti mkubwa, akisisitiza kuwa chama hicho kipo imara na kimejipanga kuhakikisha kuwa kila kura ya mwananchi inabaki salama kwa upande wa ushindi wa chama.
"Singida imeamua, Singida imesimama, na Singida ni ya CCM! Mapokezi haya makubwa ni ushahidi kwamba wananchi wanataka maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana kupitia Chama Cha Mapinduzi pekee," alisema Mlata huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliokuwa wakipiga ndera na kuimba nyimbo za hamasa.
Kwa upande wake, Ally Hapi aliwashukuru wananchi wa Singida kwa mapokezi hayo ya kihistoria na kuahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM ili wananchi waendelee kunufaika na huduma za kijamii, miradi ya maendeleo na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa shangwe na ari kubwa iliyoonekana Singida, ni dhahiri kwamba upepo wa ushindi wa CCM unaendelea kuvuma kwa nguvu mpya kuelekea mwaka 2025.
Matukio Mbali mbali kwa picha
0 Comments