MSITA AWASHUKURU NA KUWATIA MOYO WATUMISHI WA CCM WILAYA YA MANYONI

Mbunge wa Jimbo la Itigi, Yohana Msita, amewashukuru na kuwapongeza watumishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni kwa kazi kubwa na yenye tija wanayoendelea kuifanya katika kukiimarisha chama na kuhudumia wananchi.

Mbunge  Msita ametoa pongezi hizo leo Januari 09, 2026, wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za CCM Wilaya ya Manyoni, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi pamoja na viongozi wa chama hicho.


Aidha, Mbunge  Msita aliwahakikishia watumishi hao ushirikiano wa karibu kutoka kwake kama Mbunge wa Jimbo la Itigi, akibainisha kuwa yuko tayari kushirikiana nao wakati wote katika kutatua changamoto zinazojitokeza na kusukuma mbele agenda za maendeleo kwa maslahi ya wananchi.
                                   

Ziara hiyo imeelezwa kuwa chachu ya kuongeza morali, mshikamano na ari ya kazi miongoni mwa watumishi wa CCM Wilaya ya Manyoni, huku wakiahidi kuendelea kulitumikia chama kwa bidii, uaminifu na uzalendo kwa maslahi mapana ya wananchi.
Na Abdul Bandola Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments