Vijana wa Singida Wasifiwa kwa Uadilifu na Uvumilivu, Waaswa Kuendeleza Mshikamano

                                    

Vijana wa Mkoa wa Singida wametajwa kuwa ni waadilifu, wavumilivu na wenye msimamo thabiti, wasiodanganyika na vishawishi vya watu wasiojali maslahi ya umma, jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Bi. Martha Malata, aliwapongeza vijana wa mkoa huo kwa kuendelea kushikilia misingi ya uadilifu, uzalendo na kujali maslahi mapana ya jamii.

Bi. Malata alisisitiza kuwa vijana wa Singida wanapaswa kuendeleza maadili hayo kwa kuzingatia maslahi ya taifa, huku wakiepuka kushawishika na watu au makundi yenye nia ya kuvuruga mshikamano wa kijamii na maendeleo yaliyopatikana.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Singida aliwataka viongozi na wananchi kwa ujumla kuendeleza utamaduni wa kupendana, kuheshimiana na kukosoana kwa upendo pale panapotokea changamoto au makosa, badala ya kuingiza chuki, migawanyiko na mifarakano katika jamii.

“Upendo, mshikamano na mazungumzo ya kujenga ndiyo msingi wa maendeleo endelevu. Tukosoane kwa nia njema na kwa lengo la kujenga, si kubomoa,” alisema Bi. Malata.

Sherehe za miaka 49 ya CCM mkoani Singida zimezinduliwa zikiwa na lengo la kukumbuka mchango wa chama hicho katika ujenzi wa taifa, kuimarisha mshikamano wa wanachama na kuendeleza maono ya maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.

                                       




Na Abdul Ramadhani Singida


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments