Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Chief Thomas Mgonto, ameendelea kuonyesha uthubutu, uhodari na moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi baada ya kuendelea kuibana Serikali kutekeleza mahitaji muhimu ya wananchi wa jimbo hilo, hususan katika sekta ya mawasiliano.
Chief Mgonto amesema hayo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo aliwasilisha hoja yenye uzito mkubwa akiiomba Serikali kuongeza minara ya mitandao katika maeneo mbalimbali ya Ikungi Mashariki ili wananchi waweze kupata huduma bora ya mawasiliano.
Katika mchango wake, Mbunge huyo alieleza kuwa mawasiliano ni nguzo muhimu ya maendeleo ya kisasa, kwani yanarahisisha biashara, elimu, huduma za afya, usalama pamoja na shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi. Alisisitiza kuwa wananchi wa Ikungi Mashariki wanahitaji huduma ya uhakika ya mtandao ili waweze kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya taifa.
Chief Mgonto ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni sauti ya wananchi wa Ikungi Mashariki kwa kusimama imara kila mara ndani ya Bunge na kuwasemea wananchi wake kwa ujasiri mkubwa. Uwezo wake wa kujenga hoja zenye mantiki na kuzungumza kwa weledi umeendelea kuwavutia wengi, huku wananchi wakionesha imani kubwa kwake.
Wananchi wa Ikungi Mashariki wamekuwa wakimpongeza Mbunge wao kwa jitihada zake zisizokoma za kuhakikisha changamoto zinazowakabili zinafikishwa Serikalini na kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Tangu achaguliwe kuwatumikia wananchi, Chief Mgonto ameonekana kuwa karibu na wananchi wake, akisikiliza kero zao na kuzibeba kwa uzito mkubwa kwenye vyombo vya maamuzi. Hali hiyo imeendelea kumjengea heshima kubwa ndani na nje ya jimbo hilo.
Wachambuzi wa siasa na maendeleo wanaamini kuwa hoja yake kuhusu minara ya mawasiliano ni ya msingi sana, hasa katika kipindi hiki ambapo dunia imejikita katika teknolojia na uchumi wa kidijitali. Kupatikana kwa mawasiliano ya uhakika kutasaidia vijana kupata taarifa, wafanyabiashara kukuza shughuli zao, wanafunzi kujifunza kwa urahisi na wananchi kupata huduma mbalimbali kwa wakati.
Chief Thomas Mgonto ameendelea kuonyesha mfano wa kiongozi anayejali maslahi ya wananchi wake, anayefanya kazi kwa bidii na anayesimamia maendeleo ya eneo lake kwa vitendo.
Kwa hakika, Ikungi Mashariki imepata mwakilishi anayejituma, anayesikika na anayepambania wananchi wake bila kuchoka. Wananchi wengi wanaamini kuwa kwa kasi hii ya utendaji, jimbo hilo litaendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Chief Mgonto ni sauti ya wananchi, ni mtetezi wa maendeleo, na ni kiongozi mwenye maono ya kweli kwa Ikungi Mashariki.

0 Comments