Katika ziara hiyo, Mbunge. Msita amefika katika Kijiji cha Kaminyanga, ambako kabla ya kuendelea na majukumu yake ya kibunge alishiriki kutoa pole kwa wananchi kufuatia msiba uliotokea katika kijiji hicho.
Baada ya kutoka msibani, Mbunge huyo aliendelea na mkutano wa wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa ushirikiano wanaompa katika kutekeleza majukumu yake, sambamba na kusikiliza kero, maoni na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.
Mkutano huo ulitoa fursa kwa wananchi kueleza changamoto zao moja kwa moja mbele ya Mbunge, huku Mhe. Msita akizipokea kwa umakini na kuanza kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikisha viongozi na watendaji wa Serikali waliopo katika eneo hilo.
Miongoni mwa kero zilizowasilishwa ilikuwa ni ya mama mmoja ambaye alieleza kuwa mume wake, aliyewahi kufanya kazi ya ulinzi katika Ofisi ya Kijiji cha Kaminyanga, hakulipwa stahiki zake kwa muda. Kwa sasa, mzee huyo anaendelea kuugua huku familia yake ikikabiliwa na changamoto.
Baada ya kusikiliza hoja hiyo, Mbunge. Yohana Msita alichukua hatua na kuwataka viongozi husika kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi kwa wakati, akimuelekeza Mwenyekiti wa Kijiji kuhakikisha mzee huyo analipwa stahiki zake ndani ya mwezi huu.Hatua hiyo imeendelea kuonyesha namna ambavyo Mhe. Msita anavyosisitiza uwajibikaji, kusikiliza sauti za wananchi na kuhakikisha changamoto zinazowasilishwa mbele yake hazibaki kuwa malalamiko pekee, bali zinafuatiwa na hatua za kutafuta ufumbuzi.
Ziara ya Mbunge. Msita inaendelea kuwa sehemu muhimu ya kujenga daraja kati ya wananchi na uongozi, huku Mbunge huyo akisisitiza umuhimu wa viongozi kuwa karibu na wananchi, kusikiliza mahitaji yao na kushughulikia changamoto zinazohitaji hatua za haraka.
Kwa mtazamo huo, Mbunge. Yohana Msita anaendelea kuonesha mfano wa uwakilishi unaotanguliza wananchi, kwa kufika katika maeneo yao, kusikiliza kwa karibu na kufuatilia utekelezaji wa hoja zinazowasilishwa kwake.
Itigi inaendelea kupata uwakilishi unaogusa maisha ya wananchi karibu nao, sikivu na unaochukua hatua.
Na Mwandishi Wetu Singida Itigi.





0 Comments