Mgombea ubunge wa Jimbo la Itigi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yohana Msita, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisema kuwa hakuna kijiji hata kimoja katika Jimbo la Itigi kilichosalia bila kunufaika na mikono ya maendeleo ya Serikali.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, Msita alisema kuwa mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka mitano yaliyopita ni ushahidi tosha wa uongozi imara wa CCM na dira ya Rais Samia katika kuijenga Tanzania mpya yenye maendeleo ya watu wote.
Akiendelea kuzungumza, Msita aliahidi kuwa, endapo wananchi wa Itigi watampa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia, atahakikisha miradi yote iliyoanzishwa inakamilika kwa ubora na muda, sambamba na kuibua miradi mipya itakayochochea ajira, kilimo na biashara.
Alihitimisha kwa kuwaomba wananchi wote kuendelea kuiamini CCM kama chama cha maendeleo na umoja, akisema “Tukipe nguvu chama chetu, tusimame pamoja, na tuhakikishe kura zote zinakwenda kwa CCM — kuanzia Rais, Mbunge, hadi Diwani.”
Matukio mbali mbali ya Picha katika tukio hilo
Alifu Abdul Singida Itigi









0 Comments