WAZIRI KAIRUKI: HUDUMA ZA MTANDAO NA MAWASILIANO KATIKA MWENDOKASI ZINAREJESHWA

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali itahakikisha huduma za mitandao na mawasiliano katika miundombinu ya usafiri wa mwendokasi zinarejea kikamilifu kama ilivyokuwa awali.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, kuhusu kurejeshwa kwa huduma za usafiri katika njia ya Kimara, Waziri Kairuki amesema wizara yake imejipanga kuhakikisha huduma hizo zinakuwa imara na za uhakika kwa watumiaji.

Amefafanua kuwa Serikali haitakubali kuwepo kwa ucheleweshaji au mkwamo wowote utakaoathiri ufanisi wa mfumo wa usafiri wa mwendokasi, ambao unategemewa na maelfu ya wananchi jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Waziri Kairuki aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Profesa Riziki Shemdoe, ambaye pia amesema Serikali inafanya kazi kwa karibu kuhakikisha maboresho yanayofanyika ndani ya mfumo wa mwendokasi yanawanufaisha moja kwa moja wananchi.




TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments