Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Laban Kihongosi, ameendelea kuthibitisha kwa vitendo dhamira ya CCM ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, baada ya leo kwenda moja kwa moja katika eneo husika na kumaliza kero ya ardhiiliyowasilishwa jana katika mkutano wa hadhara.
Katika mkutano huo, mwananchi mzee aliwasilisha kilio yaake kuhusu mgogoro wa ardhi uliokuwa umemdhoofisha kwa muda mrefu. Kihongosi alisikiliza kwa makini, akaahidi kufuatilia, na leo ahadi hiyo imetekelezwa kwa vitendo, ndani ya saa 24 tangu kero hiyo itolewe.
Akiwa eneo la tukio, Kihongosi alishirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na wataalam husika kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi wa haki. Baada ya kero hiyo kumalizika, alimpa pole mzee huyo, akisisitiza kuwa haki ya mwananchi ni msingi wa uongozi wa CCM.
Wananchi waliokuwepo walionesha furaha na imani kubwa kwa chama na uongozi wake, wakieleza kuwa hatua hiyo ni uthibitisho kuwa CCM ni chama kinachosikiliza na kutatua matatizo ya wananchi wake bila kuwachelewesha.
Kitendo hiki Katibu Mwenezi Taifa Kenani Kihongosi kimeendelea kuimarisha imani ya wananchi kwa CCM, na kuacha ujumbe mzito kuwa ahadi za chama ni vitendo, si maneno.

0 Comments