KATIBU MKUU CCM AMPONGEZA ALIYETOA ARDHI IJENGWE SEKONDARI KATA YA KISIWANI, AFAFANUA KUHUSU ELIMU BURE

 Katibu  Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amefanya ziara katika Wilaya ya Muheza  mkoani Tanga ambapo pia amepata nafasi ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo wa ujenzi wa Shule ya Sekondari inayojengwa Kata ya Kisiwani.


Akizungumza na Wananchi akiwa katika Kata ya Kisiwani wilayani Muheza mkoani Tanga , Chongolo amesema Serikali inayosimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa kwenye eneo la elimu na kwamba ujenzi wa Shule za Sekondari unaendelea maeneo mbalimbali nchini.

"Ujenzi wa Shule za Sekondari hauko hapa Kisiwani peke yake bali unafanyika nchi nzima kwenye kila Wilaya.Shule nyingi zinajengwa zaidi ya 200 nchi nzima, kwa kutolewa fedha zote na Serikali kwa ajili ya kusogeza elimu kwa wannanchi,hiyo ndio kazi ya Serikali na bahati mbaya watu hawazisemei na kuonesha kwamba hizi shule zinajengwa na kazi kubwa inafanyika

"Lakini sisi tunapita kujiridhisha na kiwango cha ubora, kuona kama fedha zimefika, matumizi yake,huduma kama inaenda kusogezwa kwa wananchi au inaenda kupendelea eneo fulani, hapa tumejiridhisha uamuzi wa kuijenga shule hii hapa ulilenga dhamira ya kusogeza elimu kwa Wananchi,hongereni sana ,mmeniambia hapa kuhusu changamoto ya ardhi na kwa mazingira kama haya tuweka kidato cha Tano na Sita wanafunzi wetu watakuwa na uhakika wa kusoma vizuri sana ,hiii hali ya hewa inaruhusu

"Mazingira ni mazuri,hii shule iko kwenye mazingira rafiki kwa nwanafunzi kujitafutia na kutumia muda mwingi kusoma, shule inafaa iongezewe msukumo wa kuongozewa eneo ili lipatikane eneo la kuja kujenga bwalo ,kujenga madarasa mengine ya kidato cha Tano na Sita lakini kujenga nyumba za kutosha za walimu,"amesema Chongolo.

Ameongeza kuwa hivyo atakwenda kusuma ajenda ya kupata fedha Sh.milioni 130 kwenye shule zote kwa lengo la kujenga nyumba za walimu na kwamba fedha hizo zinatosha kujenga nyumba nne kwa moja badala ya kujenga nyumba moja au mbili. Ni lazima watengeneze msukumo wa kutumia hizo edha vizuri ili zienga nyumba nyingi kuliko hata ramani walizopewa.

"Hakuna ramani itakayogambana na wingi wa nyumba,nyumba zikiwa zimewekwa tatu ninyi mkaweka nyumba nne hakuna atakayekuja kuleta hoja kwanini mlijenga nyingi,shida mkipunguza mkajenga chache.Niwapongeze wananchi ninyi ni watu bingwa sana mmeonesha kwa namna mnavyoenda maendeleo.

"Hapa mmechangia zaid ya Sh.milioni 27 fedha ambazo zimetokana na nguvu kazi yenu lakini na michango yenu wenyewe kabla ya uamuzi wa Rais na Serikali anayoiongoza kuleta fedha, hongereni sana, lakini nimezungumza kujengwa kidato cha Tano na Sita ,nimesema ijengwe hapa kwasababu tayari Serikali imefanya uamuzi wa kutoa elimu bila malipo kwa kidato cha Tano na Sita ili kupanua na kuongeza wigo wa vijana wetu kupata fursa ya elimu bila malipo kuanzia darasa la awali hadi kidato cha Sita,"amesema.

Ameongeza lengo lake ni nini, wengi wanasema elimu bure maana yake hamna anayelipia lakini hiyo elimu bila malipo kwa wananchi kwasababu malipo yanatolewa na Serikali.

 "Narudia tena tunaita elimu bure tunakosea bali ni elimu bila malipo kwa maana ya mwanannchi halipi lakini Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kugharamia uendeshaji wa ile elimu badala ya mwananchi au kwa niaba ya mwananchi kwa maana kuna watu wanasema imetokea miujiza, shule zinajiendesha kwani hakuna walimu,walimu wanakuja bure shuleni? 


"Nimepata maelezo ya mzee aliyeamua kutoa ardhi kwa ajili ya elimu sio jambo dogo ni jambo la heshima basi hata jina la shule mumpe yule mzee ili iwe kumbukumbu ya kizazi na kizazi kwamba pamoja na kwamba ametoa ardhi kwa hiyari yake lakini kukumbuka ya familia kwamba hapa palikuwa kwa nani ni jina waliyoipa shule , tujenge tabia ya kuthamini anachofanya mtu, tujenge tabia ya kuheshimu na kutoa mchango na sisi kumheshimu aliyefanya kitu fulani, napendekeza hii shule iitwe Manofu Sekondari kutambua mchango wa mzee wetu Manofu ambaye ametoa ardhi yake,".Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (katikati) akiwa na ujumbe wake pamoja na mkuu wa Mkoa Mhe.Omari Mgumba (kulia) wakielekea kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
Moja ya Jengo la shule ya Kisiwani likiwa mbioni kukamilika
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo na ujumbe wake wakikagua baadhi ya majengo ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndugu Omary Mgumba (kushoto) mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ndugu Omary Mgumba (kushoto) mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kisiwani iliyopo kata ya Kisiwani wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments