UFARANSA WAANDAMWA NA MAJERUHI KOMBE LA DUNIA 2022

 Shirikisho la Soka nchini Ufaransa limethibitisha kuwa Mshambuliaji Karim Benzema atakosekana kwenye Michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Qatar baada ya kupata majeruhi akiwa kwenye mazoezi.


Mshindi huyo wa Tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka huu wa 2022 ameondolewa kwenye Kikosi cha Mabingwa hao watetezi wa Michuano hiyo na atakaa nje kwa wiki tatu kuuguza majeraha yake.

“Benzema atakosekana kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2022, kwa sababu ya majeruhi, tulienda kuangalia vipimo vya MRI hapa Hospitali ya Doha, tulijiridhisha kuwa kweli amepata majeruhi”, taarifa ya Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF).

Kupitia ukurasa wake rasmi wa ‘Instagram’ Benzema, ameandika: “Katika maisha sijawahi kukata tamaa, lakini kwa usiku huu nimefikiria sana timu yangu, sababu hizi (majeruhi) zimenifanya kuondoka kwenye timu na kumpisha mwengine atakayesaidia timu kwenye Kombe la Dunia 2022, nashukuru kwa ujumbe wenu kwangu.”

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema: “Ni huzuni kwa Karim ambaye alikuwa na malengo makubwa kwenye Kombe la Dunia 2022. Bila shaka naamini timu yangu, tutafanya kila linalowezekana kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kuelekea kwenye Michuano ya Kombe la Dunia.”

Hadi sasa, timu ya taifa ya Ufaransa imethibitishwa kuwakosa Nyota wake muhimu takribani sita katika Michuano hiyo mikubwa ambayo inaanza kutimua vumbi Novemba 20 hadi Desemba 18 mwaka huu nchini Qatar.

Nyota hao watakaokosekana kwenye timu hiyo ya taifa kwa sababu ya majeruhi ni Karim Benzema, Paul Pogba, Christopher Nkunku, Mike Maignan, N’Golo Kanté na Presnel Kimpembé.


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments