RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA WAKUU WA NCHI SADC ORGAN TROIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB) Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023. Mkutano huo utajadili hali ya Usalama Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB) Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023. Viongozi wengine katika picha ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Tshisekedi, Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob, Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa pamoja na Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakati Wimbo wa Taifa wa Namibia pamoja na ule wa SADC ukiimbwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB) Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments