Waleta mbinu kupoza makali makato huduma za kifedha mtandaoni

 Makato ya huduma ya kifedha yanatajwa kuwa chanzo cha Watanzania wengi kuikimbia njia hiyo ili kupunguza ukali wa maisha na kuanza kutumia njia nyingine mbadala katika kutuma na kupokea fedha.

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha wastani wa Mtanzania kufanya miamala kwa njia ya simu imepungua kutoka miamala 106 mwaka 2021 hadi miamala 102 mwaka 2022.

Mkurugenzi wa kitengo cha mauzo na Masoko wa kampuni ya huduma za fedha mtandaoni, Azam Pesa, Gillian Rugumamu juzi Juni 9, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo amesema lengo lao ni kupunguza makali ya huduma hizo kwa kuwezesha kutuma na kupokea pesa bure.


"Mfumo wake unaruhusu wateja kutoka mitandao yote ya simu kujiunga na kutumia huduma ya AzamPesa kwa watu wote wenye namba za simu za mkononi bila kubagua na kwa kiwango chochote," amesema

Amesema huduma ya kutuma na kupokea bure imeanzishwa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wao na wanaimani itakuwa chachu kwa Watanzania wote siyo wateja wa Azam Pesa kuanza kutumia huduma hiyo salama, rahisi na uhakika.

"Tunatarajia kuona watanzania wote wanachabgamkia huduma ya kuishi maisha bila makato na wateja watakao tumia huduma hii wataokoa Sh5,400 kuanzia Sasa," amesema Rugumamu

Amesema taasisi hiyo imejiwekea mikakati ya kuendelea huduma bora nchini kote ambapo imejikita zaidi kuongeza mawakala Ili kuwafikia watanzania wote

Kwa upande wake Fredrick Michael, msimamizi mkuu wa huduma ya AzamPesa amesema matarajio yao ni kuwafikia Watanzania  wote na kwamba huduma zao zimesambaa nchi nzima.

Naye Rehema Salim, Afisa Uhusiano wa Makampuni ya Bakhres Group alitoa wito kwa Watanzania wote kuchangamkia fursa hiyo kwani kutuma na kupokea fedha bila makato inawezekana.


Joseph Meshack, mkazi wa Buguruni amesema huduma za kifedha ni muhimu hasa za mtandaoni lakini kutokana na wingi wa makato huzikimbia na kufanya njia mbadala.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments