Bashe aitaka CBT kuunda tume huru

MTWARA: WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameigiza Bodi ya Korosho Nchini (CBT) kuunda tume huru ikiongozwa na Ofisa wa usalama wa taifa kuchunguza madai ya kuwepo changamoto ambazo zinasabisha athari hasi kwenye uuzaji wa korosho ghafi nchini.

Bashe ametoa agizo hiloNovemba 27, 2023 baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wenyeviti wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mtwara, Lindi na Ruvuma wakilalamikia changamoto nyingi ikiwemo mnada awali kuangusha bei korosho, usafirishaji wa korosho usiku na suala la utiriri wa maghala.

Amemtaka Mkurungezi wa CBT, Francis Alfred kuhakikisha tume hiyo inaundwa leo na kufanya kazi ndani ya siku 14 na kuwasilisha ripoti wizarani kwa ajili ya hatua zaidi.

Akiongea kwa njia ya simu na Mkurungezi huyo, Bashe amemtaka mwenyekiti wa hiyo tume kuwa mtu wa usalama wa taifa, na baadhi ya wajumbe wakiwa ni wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

“Nataka mwenyekiti wa hiyo tume awe mtu wa Usalama wa taifa na hiyo tume ifanya kazi ndani ya siku 14,” amesema.

Amesema tume hiyo inatakiwa kuchunguza malalamiko yote ambayo yanasabisha kuanguka kwa bei ya korosho nchini.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments