MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), imeyataka mabasi ya usafirishaji mikoani kuzingatia muda wa kuchimba dawa kuwa ni dakika 20 badala ya 10.
Agizo hilo limetolewa jijini Arusha na Mkurugenzi wa LATRA, CPA Habibu Suluo katika Mkutano na waandishi wa habari.
“Kusimama eneo la huduma kwa walau dakika 20. Mambo ya kuchimba dawa dakika 10 hakuna.”
Amewataka wasafirishaji kutoacha abiria wakati kuchimba dawa, pia wazingatie usafi wa basi ikiwemo kumwagilia dawa za kuua wadudu pia kuweka vifaa vya kuhifadhi taka.
0 Comments