WANANCHI IKUNGI WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA, WANAFUNZI WAKWAMA KWENDA SHULE.

Wananchi wa Kijiji cha Kipunda, Kata ya Mtunduru Wilayani IKUNGI Mkoani Singida wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa Barabara na kusababisha Wanafunzi kushindwa kwenda Shule kipindi cha Masika.

Wananchi hao waliwasilisha kero hiyo ya barabara katika Mkutano wa hadhara kijijini hapo, Kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA akiwa katika Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.

Walisema kuwa kipindi hiki cha Masika baadhi ya wanafunzi wanashindwa kwenda shule, pale baadhi ya Makorongo yanapojaa  maji na kushindwa kuvuka.

Aidha walisema kuwa baadhi ya wazazi wanalazimika kuwapeleka na kwenda kuwachukua watoto wao shule, wakihofia usalama wa watoto wao kwenye kuvuka Maji.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Ikungi ALLY MIMBI alisema, tayari wamepata mkandarasi wa kujenga barabara hiyo na kuondoa changamoto hiyo iliyopo katika baadhi ya maeneo ya barabara hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida PETER SERUKAMBA alisema serikali itazitatua changamoto hizo kwani tayari fedha zimetengwa kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo ili iweze kupitika.

SERUKAMBA alimtaka pia Meneja wa TARURA Wilaya ya Ikungi kuhakikisha wanaitatua changamoto hiyo ya barabara ili kurahisisha mawasiliano ya barabara katika Kata ya Mtunduru.



Na RAFURU KINALA ,SINGIDA


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments