Bi Martha Mlata Amtembela Mwenyekiti Wa Kwanza Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Wa Singida.

Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Singida Timoth Zakaria Kingu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia Haki na Maslahi ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

Mzee Kingu ambae alipata pia kuwa mkuu wa wilaya ya Manyoni, amesema hayo nyumbani kwake mjini Singida alipotembelewa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Martha Mosses Mlata kumjulia hali na kupata maoni yake kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dr Samia Suluhu Hassan ambae ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Katika mazungumzo yake, mzee Kingu amesema hatua kubwa zinazochukuliwa na Rais za kuwatetea Wanyonge zinaharakisha kuwaletea Wananchi maendeleo, hatua ambazo zinaendana na maono ya Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhakikisha kila mtu anafaidika kutokana na keki ya Taifa.

Akizungumza na  Mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chama mkoa wa Singida Timoth Zakaria Kingu ambae ni mwanzilishi wa Ujenzi wa Ofisi za Chama mkoa na Uwanja wa Michezo wa CCM Liti, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Martha Mosses Mlata amesema CCM inafarijika na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wake.

Mlata alifika nyumbani kwa mzee Kingu akiambatana na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa huo Ahmed Athuman maarufu Kaburu ikiwa ni kufufua utaratibu ambao umeanza kusahaulika wa kuwatembelea Wazee na Waasisi wa Chama na Serikali mkoani humo.

Habari Picha Na Matukio Mbali Mbali Yaliyoendelea Katika Ziara Hiyo Ya MwekitiWa CCM Mkoa Wa Singida Bi Martha Mlata Alie Ambatana  Na Katibu Mwenezi Wa CCM  Mkoa Kwenda kumtembelea Mwenyekiti Mstafu Nyumbani Kwake Bw. Tomothy Kingu.  Na Abdul Bandola  Singida.TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments