RC. Singida aiomba Serikali kuweka kodi Mafuta ya kupikia kutoka nje ya...

         
                      
Akisisitiza jambo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kurudisha kodi ya mafuta ya kula yanayoagizwa kutoka nje ya nchi.

"Tukiweka kodi, maana yake tutaweza kushindana, alizeti zetu zitapanda bei," amesema Serukamba wakati akizungumza kwenye mkutano huo.

Ameongeza kwamba serikali imehamasisha wananchi kulima, imetoa ruzuku ya pembejeo na mikopo ya mbegu, lakini wanakatishwa tamaa na hali ya bei ya alizeti ambayo haiendani na gharama za uzalishaji.

Serukamba amesema Singida wamelima ekari 600,000 za alizeti, maana yake zikivunwa, asilimia 44 ya mafuta ya kula nchini yatatoka mkoani humo.


Akizungumzia hoja hiyo, Chongolo amesema amelichukua, atakwenda kujadiliana na wenzake kuona namna bora ya kulitatua ili wakulima waendelee kuzalisha kwa faida.

"Tumehamasishana kulima, tumelima. Hatuwezi kuhamasisha wawekezaji wa nje wakati wa ndani hawanufaiki. Hili nimelibeba, ngoja tukajadiliane na wenzangu huko," amesema Chongolo huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments