DTB YAENDELEZA UBABE CHAMPIONSHIP, YAICHAPA 1-0 PAMBA UWANJA WA CCM KIRUMBA

TIMU ya DTB imeendeleza wimbi la ushindi katika ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao, ijulikanayo kama Championship baada ya kuwachapa wenyeji, Pamba SC 1-0  Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao pekee la DTB leo limefungwa na mshambuliaji Mghana, Nicholas Gyan dakika ya 57 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 33 na kuendelea kuongoza Championship kwa pointi nne zaidi ya Ihefu SC baada ya wote kucheza mechi 13.
Jahazi la Pamba linazidi kuzama, sasa wakibaki na pointi zao 16 za mechi ya 13 katika nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu16 na sasa badala ya kuwania kupanda Ligi Kuu, wanahitaji kupambana wasishuke.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments