Shule na wanafunzi 10 bora Kitaifa Matokeo ya Upimaji Darasa la Nne,Twibhoki ya mkoani Mara yaziburuza shule zote 14,144

SHULE ya Msingi Twibhoki iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya, kimkoa na Kitaifa katika matokeo ya upimaji wa darasa la nne 2021.

Kiwilaya ni nafasi ya kwanza kati ya shule 108, kimkoa ya kwanza kati ya 761 na Kitaifa ya kwanza kati ya shule 14144.

Hayo yamejiri leo ambapo Baraza la Mitihani (NECTA) pia limetangaza matokeo Kidato cha Nne,QT, Kidato cha Pili na matokeo haya ya upimaji wa Kitaifa wa darasa la nne na Kidato cha Pili 2021. Tazama matokeo yote hapa>>>

Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 15,2022 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), Dkt. Charles Msonde jijini Dar es Salaam.

Shule 10 bora kwenye upimaji wa darasa la nne 

1. Twibhoki - Mara
2. Graiyaki - Mara
3. St. Peter Claver - Kagera
4. Green Star - Shinyanga
5. Kwema Modern - Shinyanga
6. Kikodi - Ruvuma
7. Bohari - Kagera
8. Rocken Hill - Shinyanga
9. Musabe - Mwanza
10. Mtuki - Dar es salaam

Watahiniwa 10 bora matokeo darasa la nne

1. Joel Leonard - Libermann 
2. Falima Mwenura - Green Star Junior
3. Goodluck Mtaki - Green Star Junior 
4. Careen Slaa - Sasa
5. Joyce Ndonde - Wonder Kids
6. Samirah Mnali - Wonder Kids
7. Jonathan Maziku - Green Star
8. Balkis Majowe - Wonder Kids
9. Christopher Kileo - Green Star
10. Doreen Sanare - St Francis De Sale

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments