Russia yauvimbia Umoja wa Mataifa, yakataa kusitisha uvamizi Ukraine

Serikali ya Russia imekataa kutii amri ya mahakama ya juu ya Umoja wa Mataifa ya kusimamisha uvamizi wake nchini Ukraine baada ya majaji hao wa The Hague kutangaza uamuzi wao.

Hatuwezi kuutekeleza uamuzi huu," msemaji wa serikali hiyo ya Kremlin, Dmitry Peskov alisema, akiongeza kuwa pande zote Russia na Ukraine walitakiwa kukubaliana jinsi ya kutekeleza uamuzi huo.

"Hakuna kuridhia kunakoweza kuonekana katika shauri hili," alisema Peskov.  

Mahakama ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa jana (Jumatano) iliamua kuwa Russia isimamishe "mara moja shughuli zake za kijeshi ilizozianza Februari 24 ndani ya mipaka ya Ukraine."

Ukraine iliishtaki Russia kwenye mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa baada ya Rais Vladimir Putin kuanza uvamizi huo wa kijeshi.

Peskov alidai kuwa ujumbe wa Russia katika mazungumzo hayo na serikali ya Kyiv kwa ajili ya kumaliza vita "ulikuwa unaonyesha utayari kwa kiwango kikubwa kuzidi wenzao katika majadiliano".


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments