RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALI MBALI NA WATAAPISHWA 19 SEPTEMBA 2024

 

RAIS  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

Bi. Nenelwa Mwihambi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Mwihambi alikuwa Katibu wa Bunge; na

Bw. Baraka Ildephonce Leonard ameteuliwa kuwa Katibu wa Bunge. Bw. Leonard anachukua nafasi ya Bi. Mwihambi ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Viongozi walioteuliwa wataapishwa tarehe 19 Septemba, 2024 saa 09.00 alasiri, Ikulu – Dar es Salaam.

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments