Ludewa:Wachimbaji Wadogo Wa Dhahabu Waomba Leseni

 Wachimbaji wadogo wa madini aina ya dhahabu katika Kitongoji cha Nyamaramba kijiji cha Ibumi kata Ya Ibumi wilayani Ludewa mkoani Njombe wameomba serikali kuwasaidia vijana kupatiwa Leseni ya Kumiliki Vitalu vya Kuchimba dhahabu ili kuondokana na Mgogoro uliopo kati ya Moja ya Wamiliki wa Leseni aliye Hodhi moja ya kitalu katika Eneo Hilo.


Wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Ibumi akiwemo Kelvin Mbombo na Jeremia Haule mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa wamefikia hatua hiyo ya kuiomba Serikali Kuwasaidia kumiliki leseni za uchimbaji wa Madini kutokana na baadhi ya Wananchi wa Kijijji hicho kujishughulisha na Uchimbaji wa huku wengine wakijishughulisha na Kilimo.

“Waakati mwingine tunafuatwa na mapanga tunatishiwa,kule kuna mashimo zaidi ya sabab na yote yamesimama mtu anakwambia sahizi sio wakati wakufanya kazi”alisema Kelvin Mbombo

Aidha wameiomba serikali kuwafikishia soko lamadini wilyani Ludewa ili kurahisisha kusafiri umbali mrefu kufuata soko lililopo mjini Njombe

Kutokana na Malalamiko ya wachimbaji wadogo wa kijiji hicho Kumlalamikia Mmoja ya Wawekezaji wa Kitalu kijiji hapo mmoja wa wakeaji ambaye pia ni mchimbaji mdogo bwana Filibeth Kosimasi Kayombo amesema.

“Mimi nimeanzisha leseni mwaka jana baada ya kuaznisha nikawa mgonjwa sasa wakati wananchimba wakawa wanatorosha madini mengi sana na waliotorosha ndio hao hao wanaolalamika ndio kisa mimi cha kusimamisha mgodi niangalie utaratibu na baadaye pia ilifika mahalia ule mgodi walitaka kuua”alisema Fiibeth Kosimasi Kayombo

Joseph Kamonga ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Amewataka Wachimbaji Hao Wadogo Kujiunga Katika Vikundi ili Kupatiwa Leseni na Kumtaka Afisa Madini Kifika Kijijini hapo kuwasaidia wachimbaji hao kupata leseni pamoja na kuwataka wamiliki wa vitalu kuviendeleza.

“Na mara nyingi wanaogundua kuwa kuna madini ni wachimbaji wadogo ila wengine wanakuwa hawajapewa elimu na namna ya kupewa leseni.Hii tusitumie kama nafasi kuwanyonga vijana”alisema Kamonga


Mbunge wa jimbo la Ludewa wkili Joseph Kamonga akizungumza na wanannchi wa kitongoji cha Nyamalamba kijiji cha Ibumi alipofika katika eneo hilo ili kuzungumza nao namna utekelezaji wa ilani ulivyofanyika tangu alipochaguliwa pamoja na kupokea changamoto zao.

Baadhi ya wananchi wa Ibumi wakimsikiliza mbunge wao mara baada ya kuelezea changamoto zao zinazowakabili ikiwemo umeme,barabara bei za mahindi na uchmbaji wa dhahabu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments