Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watendaji wa Serikali kuweka utaratibu wa kufuatilia kero zinazowakabili wawekezaji na kuzitatua.
Mhe. Rais ametoa agizo hilo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha.“Tunavuta wawekezaji wanakuja lakini wakifika na wakishajenga viwanda, tusiwaache wenyewe, tufuatiliena tujue kero zinazowakabili na tuzitatue,” ameagiza Rais Samia.
Tangu alipoingia madarakani Machi 19, 2021 Rais Samia amekuwa akichukuwa jitihada mbalimbali za kuwavutia wawekezaji na kuhakikisha wale waliopo wanaendesha shughuli zao kwa kufuata sheria bila kubughudhiwa.
Na Ahmed Sagaff – MAELEZO
0 Comments