Mamia ya wakazi wa Jiji la Mbeya wamejitokeza kwa wingi katika Kata ya Nsalaga Jijini Mbeya kumpokea Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson huku Machifu wakitoa neno la baraka na kumlinda.
Dk Tulia ambaye amewasilia Mkoani Mbeya Leo Jumamosi ,Februali 26, majira ya saa 9.45 alasiri.
Mara baada ya kuwasili alipokewa na Machifu wakiongozwa kiongozi wa machifu Mkoa wa Mbeya ,Rocket Mwanshinga viongozi wa Serikali na Chama akiwepo msanii wa kizazi kipya kutoka Rebo ya Wasafi, Raimond Mwakyusa (Rayvann).
Akizungumza mara baada ya kumpokea Spika Chifu Mwanshinga amesema kuwa Dk Tulia amerudi nyumbani na wako naye hawatamuacha kwani ni mtoto wao wamemkuza na kukemea mabaya yatakayothubutu kujitokeza.
''Tulia wewe ni mwanetu umekuja nyumbani tutakulinda na tunakemea mabaya yote mabaya juu yako ''amesema.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya, Aran Mwaigaga amesema kuwa Tulia ni Lulu na dhahabu ya Mkoa wa Mbeya na mhimili wa Bunge na mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM ni wakati wanachama waweke tofauti zao pembeni na kuweka Maendeleo ya Mkoa mbele.
'Nasema hivyo namaanisha kwani Mkoa wa Mbeya Tangu nchi ipate Uhuru ni historia ya kipekee kuwa na Mbunge na Spika Mwanamke sasa ni wakati wa kutumia ili Jiji liwe la kisasa na kijani''amesema.
Amesema kuwa ni wakati sasa chama kimefika hatua kiliyokuwa kikistahili kwa kuleta tija ya kukijenga kwa kuwa wamoja na kuunga mkono juhudi za Spika Dk Tulia Ackson kwani wakati wa Maendeleo umefika.
Mkazi wa Uyole, Jane Samson amesema kuwa mapokezi ya Spika na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ni kufuru kwani wameacha shughuli za kiuchumi na kuungana na wanambeya katika mapokezi.
0 Comments