Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema CCM inadridhishwa na juhudi za kisera zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika medani za kimataifa.
Akizungumza leo Februari 20 katika uwanja wa zamani wa ndege, katika mapokezi ya Rais Samia aliyerejea kutoka barani Ulaya, Shaka amesema kazi inayofanywa na kiongozi huyo sio ndogo, kwani amefanikiwa kuithibitishia dunia msimamo wa taifa, sera za serikali yake kama fahari kwa Afrika.
"Rais Samia kila alipopita amekutana na wakuu wa nchi wenzake, pia alikutana na makundi mbali mbali na kutoa hotuba za kizalendo akiweka msisitizo wa mashirikiano ya kikanda na kimataifa na kumfanya ajipambanue kimataifa.
"Rais Samia ni alama mpya ya Nchi yetu na kioo cha Afrika kwenye medani za kimataifa. Amekuwa mchapakazi anayesimamia utekelezaji wa sera zilizomo kwenye ilani ya Uchaguzi," amesema Shaka.
Amesema CCMtangu awali haikukosea kumfanya kuwa Makamu wa Rais na sasa ni Rais.
“CCM hakina hofu naye hata aliposhika urais baada ya kifo cha Hayati Dk John Magufuli. Watanzania wamejawa furaha na matumaini kadri wanavyomuona kingozi wao akihangainja huko na huko.
“Amefanikiwa kukubalika kimataifa pia akikiniwa na jumuiya za kimataifa, taasisi za fedha na mashirika ya kimaendeleo," amesema shaka.
Amesema Sera ya Mambo ya nje ya Tanzania imelenga kuendeleza diplomasia ya uchumi baada ya kupata mfanikio makubwa ya kujitangaza mimataifa, kuelezea sera na misimamo yake tokea awamu ya kwanza hadi ya sita.
Shaka ameongeza kusema Rais samia amejenga ukuribu na viongozi wa mataifa yenye uchumi imara duniani baada na kufanikiwa kukutana na marais wenzake kadhaa kutokana na msingi uliowekwa watangulizi wake.
"Rais Samia itakumbukwa alianza kuzuru nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla hajatembea mataifa ya Ulaya na Marekani. Amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia kukutana na jumuiya za kimataifa," ameeleza shaka.
0 Comments