Vijana mkoani Singida wametakiwa kujiamini, kuonesha na kuvitumia vipaji walivyonavyo katika kuleta ubunifu na ugunduzi wa mambo kwa kuwa wengi wana vipaji lakini hawajavitambua.
Akieleza umuhimu wa vijana kutumia akili zaidi kuliko elimu DC Muro amesema kwamba duniani wagunduzi wakubwa hawakutumia elimu lakini walitumia akili na wakafika mbali hivyo kuwataka wajitume na waweze kutumia vipaji vyao kama njia ya kupitisha elimu wanazopata.
Aidha Mkuu wa Wilaya Muro amebainisha kwamba kijana anayemaliza chuo na kukaa mtaani akisubiri Serikali itoe ajira ni matokeo mabaya ya matumizi ya vipaji kwa kuwa kila mmoja amepewa kipaji chake.

Amewataka vijana kujiunga katika vikundi na kuvisajili ili waweze kupata mikopo kupitia asilimia Nne katika Halmashauri zao huku akiwakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa msaada wa mawazo kwa vijana wenye vikundi.
Muro ameendelea kusema kwamba huenda matumizi mabaya ya simu janja ndio chanzo cha vijana kushindwa kufikiria vizuri namna ya kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ugunduzi wa vipaji vyao na namna ya kupata mitaji na utajiri kwa ujumla.
Amewataka vijana kutumia Kongamano kuzitumia fursa ambazo zimekuwa zikioneshwa katika mada mbalimbali zilizowasilishwa, na kila mwenye kipaji kuanza kuzitumia.
Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida na mratibu wa Kongamano hilo Frederick Ndahani amesema lengo la Kongamano hilo ni kuonesha fursa za kiuchumi ambazo zimezunguka Mkoa wa Singida ili waweze kuzitumia na kujikwamua katika maisha yao ya kila siku.
Aidha akieleza jitihada za Serikali katika Mkoa wa Singida zakuwainua vijana amesema katika kipindi cha mwaka 2018/2022 Mkoa umetoa jumla ya Tsh. Milioni 601.4 ikiwa ni mikopo iliyotolewa katika viku
0 Comments