Amesema, hivi sasa hakuna mgonjwa yeyote wa corona aliyelazwa hospitalini nchini Uganda, lakini bado kuna watu wenye ugonjwa huo nchini humo na hilo linafanya hatari ya kuzuka wimbi jingine kuwa kubwa la maambukizi ya UVIKO-19.
"Tunapaswa kuchukua tahadhari kubwa hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi ya nchi bado zina karantini ya corona kutokana na kuzuka upya wimbi la maambukizi ya ugonjwa huo," amesema kwa kusisitiza.
Takwimu za karibuni kabisa za Wizara ya Afya ya Uganda zinaonesha kuwa, katika kipindi cha baina ya tarehe 12 hadi 14 mwezi huu wa Aprili, kuliripotiwa kesi 27 za corona nchini humo. Kiwango hicho ni cha maambukizi ya chini kabisa ya asilimia 0.3 ikiwa na maana kwamba janga la corona limedhibitiwa nchini Uganda. Viwango vya kimataifa vinasema kuwa, kesi za ugonjwa wowote zilizo chini ya asilimai 5 huwa na maana janga la ugonjwa huo limedhibitiwa.
0 Comments