![]() |
Mtoto akipata chanjo ya surua |
Jumatano iliyopita Umoja wa Mataifa ulitangaza ongezeko la asilimia 80 la maambukizi ya surua kote duniani katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu hilo likiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na muda sawa na huo mwaka jana.
Kwa mujibu wa ripoti za Shirika la Afya Duniani na Shirikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, surua imeongezeka sana barani Afrika kutokana na ukosefu wa usawa katika kusambaza chanjo.
![]() |
aarifa zinasema kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la ugonjwa wa surua barani Afrika tokea mwanzo wa mwaka huu wa 2022. |
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kumeripotiwa kesi zaidi ya 17,300 za maambukizi ya surua duniani kote katika miezi ya Februari na Machi mwaka huu. Hii ni katika hali ambayo mwaka jana katika kipindi sawa na hicho maambukizi yalikuwa 9,600
WHO inasema nchi za Afrika ndizo zinazoongoza katika maambukizi hayo mapya ya surua.
WHO inabaini kuwa surua ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika kwa kupokea chanjo na kwamba mabilioni ya watoto hupokea chanjo dhidi ya ugonjwa huo unaoambukiza kwa njia ya hewa. Kila mtoto anahitaji kupokea dozi mbili za chanjo dhidi ya surua, ugonjwa ambao huenea kwa kasi kubwa zaidi kuliko Ebola, homa au corona.
0 Comments