Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro amewaongoza watoto katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa katika viwanja vya shule ya msingi Puma
Akizungumza katika maadhimisho haya Dc Muro amesema Ikungi tutamlinda mtoto na kutengenezea mazingira wezeshi na bora ya kupata haki zake za Msingi
Amewataka wazazi kutumia muda na familia zao haswa watoto katika kuhakikisha wanawalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa na kusisitiza jukumu la kulinda mtoto ni la kila mzazi
"Tuimarishe ulinzi wa mtoto, tokomeza ukatili dhidi yake. Jiandae kuhesabiwa."
Imetolewa ofisi ya mkuu wilaya ikungi
0 Comments