Akizungumza leo Alhamisi Juni 20,2022 Spika Dk Tulia amesema katika mjadala huo wa bajeti kuu ya Serikali zinajadiliwa hoja za kila wizara na kila wizara itapewa fursa ya kujibu hoja zake.
“Waheshimiwa mawaziri mliopo, naomba muwaite na mawaziri walioko Dodoma ambao hawana ruhusa ya kutokuwepo bungeni na hawajasafiri na mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan) na hawajasafiri kwenda popote waje bungeni,”amesema.
Amesema bajeti kuu ni bajeti ya Serikali yote na kila mmoja anatakiwa kuchukua hoja zake zinazojadiliwa bungeni.
0 Comments