
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Cheti kwa Mshindi wa Jumla kwenye Mafunzo ya Awali Kozi Na. 1,2022 ya Jeshi la Uhamiaji Konstebo Geofrey Felician Zakaria, wakati wa Ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyoshirikisha jumla ya Wahitimu 818 katika Chuo cha Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga tarehe 15 Agosti, 2022.
Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali ya Askari wa Jeshi la Uhamiaji Kozi na. 1/2022, katika Chuo cha Uhamiaji cha Boma Kichakamiba.
Aidha, Rais Samia amesema Idara hiyo haina sababu ya kuchelewesha wageni kupata vibali vya kuingia nchini kwa kuwa wanatumia mifumo ya kisasa ya kielektroniki katika utoaji wa vibali hivyo.
Vile vile, Rais Samia amemuagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala kuwarudisha mafunzoni Maafisa na Askari waliopo kazini kupata mafunzo tena chuoni hapo.
Pia, Rais Samia ametaka kuwepo kwa mafunzo baina ya vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini ili kupata uzoefu wa pamoja.
Rais Samia amelitaka Jeshi la Uhamiaji kubuni njia mbalimbali zitakazosaidia kuimarisha utendaji ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia na mbinu mpya za uhalifu zinazojitokeza.
Haya ni mafunzo ya kwanza kwa Uhamiaji tangu kuanza kujitegemea kwa Jeshi hilo ambapo Askari wa uhamiaji 818 wamehitimu na mafunzo hayo kupewa jina la Operesheni Ujenzi.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
0 Comments