Pcha Ni Wakati Wa Kuhesabu Kura baada ya Uchaguzi Mdogo Uliofanyika katika baraza hilo
![]() |
Omary Hamisi Akiongea na Viongozi Wenzake Wa Kamati Ya Utekelezaji Ya Jumuiya Ya Wazazi Mkoa Wa Singida ,Tayari Kwa Kuendelea Kutekeleza Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Wa Singida. |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida, Bi.Bertha Nakomolwa akizungumza katika Kikao Cha Baraza la wazazi na Kamati ya utekekezaji Ya Jumuiya Ya Wazazi Mkoa Wa Singida.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida, Bi.Bertha Nakomolwa akipata picha ya pamoja na Viongozi wa kamati ya Utekelezaji Wa Baraza la Wazazi Mkoa Wa Singida.
Uongozi wa Kamati ya Utekelezaji wametakiwa kuendeleza mshikamano na ushirikiano ili kuhakikisha kazi zinatendeka kupitia Ilani ya CCM ili wanachama na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na imani na Chama hicho.
Ameyasema hayo leo Januari 12,2023 Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Wazazi CCM Mkoa wa Singida . Bi.Bertha Nakomolwa Katika Balaza la wazazi lilofanyika offisi Za CCM Mkoa Wa Singida.
Amesema kuna umuhimu wa viongozi wa chama hicho kuhakikisha kamati ya Siasa kutoa hamasa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha Chama hicho kinafanya vizuri katika chaguzi zijazo.
Aidha Bi.Bertha Nakomolwa amewataka viongozi hao kushuka kwenye kata, wilaya na matawi kutoa elimu kuhusu masuala ya chama hasa Ilani ya Chama na utekelezaji wake katika maeneo mbalimbali kwenye mkoa wa Singida
Amesema kuna changamoto ya upatikanaji wa kadi za uanachama ingawa wanachama wengi wanaingia kwenye chama hicho hivyo ameshalifikisha kwenye uongozi wa juu na linashughulikiwa.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Bi Lucy Shee amewasihi kamati ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi kuhakikisha wanatumia michango kutekeleza miradi mbalimbali ili Juhudi za Jumuiya ya Wazazi zionekane na wanachama kuwa na imani na Chama hicho.
Katibu wa CCM Mkoa wa SingidaBi. Lucy Shee Amewataka viongozi wa kamati ya Utekelezaji kuwa kiungo kwa wazazi wote wa Mkoa wa Singida na kwa wananchi wa mkoa huo kwani ndani yenu wamo vijana, wanawake,hivyo wametakiwa kuhakikisha Chama kinakuwa imara.
0 Comments