Rais Samia aliyeingia madarakani Machi 19, 2021 akirithi mikoba ya hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 wakati akipatiwa matibabu Dar es Salaam.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Ikulu Dar es Salaam, Januari 3, 2023 katika kikao cha Rais Samia ambaye ni mwenyekiti wa CCM na viongozi wa vyama vya siasa 19 vyenye usajili wa kudumu akisema hivi sasa kumeshuhudiwa mahusiano mazuri ya viongozi wa vya
“Hata leo tumeshuhudia katika chombo kimoja cha habari ikionyesha viongozi wa vyama siasa kule mkoani Iringa, akiwemo Richard Kasesela (mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM) mchungaji Peter Msigwa (Mjumbe wa kamati kuu Chadema) na Peter Ndolezi (mjumbe wa baraza Kuu la ACT), wakisimama kuunga mkono jitihada za Rais kuhusu uhifadhi wa mazingira.
“Kwa kitendo kile au tukio lile sasa tunaanza kushuhudia tukisimama pamoja kwa masilahi ya Taifa letu, sisi tupo tayari kuyafanyia kazi maelekezo utakayoyatoa,” amesema Majaliwa.
0 Comments