JESHI la Polisi Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wameahiriki kufanya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wananchi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza baada ya kushiriki kwenye usafi,Kamanda wa Polisi Wilaya ya Same SSP Phinias Majula asema wao kama jeshi la polisi wameona ni vyema kushirikiana na jamii kwenye kusafisha mazingira kuepuka milipuko ya magonjwa kama kipindupindu, lakini mazingira yanakuwa safi na salama.
Aidha ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira ili yawe safi huku akitumia nafasi hiyo kuomba jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taharifa za uhalifu katika wilaya hiyo, kwani ni jukumu lao kuwalinda wananchi na mali zao.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Mji Mdogo Wilaya ya Same akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Anastazia Tutuba ametoa shukrani za dhati kwa Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi kwenye shughuli za kijamii.
pia ameliomba kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na wananchi kwa lengo ni kujenga usiano mzuri baina ya jeshi na wananchi.

Chanzo Michuzi
0 Comments