KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Daniel Chongolo ameelezwa namna wakulima katika Kata ya Kiloka, Halmashauri ya Morogoro Vijijini ambavyo wamedhamiria kuingia kwenye soko la ushindani wa mazao ya viungo.
Akizungumza leo Februari 3,2023 mbele ya Katibu Mkuu wa CCM ambaye yupo kwenye ziara mkoani Morogoro, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Dkt Hamis Taletale amesema pamoja na kupokea fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo lakini wakulima wa jimbo hilo wameweka dhamira ya kushindana na wenzao wa upande wa Zanzibar katika soko la Dunia kwenye kilimo cha mazao ya viungo" Amesema Dkt Taletale.
Awali Babu Tale amemueleza Katibu Mkuu wa CCM kwamba wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwani wameendelea kupokea fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kwamba wananchi wa jimbo hilo wameshaamua ikifika mwaka 2025 kura zote ni kwa Rais Samia.
Chongolo yuko mkoani Morogoro kwenye ziara yake ya siku tisa akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa haji Gavu.
0 Comments