Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza na Mwananchi Digital kuhusu mkakati wa uboreshaji elimu kwenye wilaya hiyo.
Ndemanga amesema wameandaa kikosi kazi ambacho kitapita kila nyumba kwa lengo lakuwasaka wanafunzi kidato cha kwanza wasiofika shuleni hadi sasa na watoro wa kudumu.
Amesema watendaji wa kijiji na kata watashirikishwa kwenye kampeni hiyo ya kawasaka watoto shule za msingi na sekondari na wale wasio fika shuleni mpaka sasa.
Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Lindi, Rehema Nahale amesema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mwamko mdogo wa wazazi kuhusu masuala ya elimu, upungufu wa walimu 214 wa shule za msingi na 111 shule za sekondari, umbali mrefu kutoka nyumbani kwenda shuleni na kurudi.
"Sisi kama idara ya elimu tuna jitahidi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi waone umuhimu wa elimu," amesema Rehama.
Nahale amesema mwaka wa masomo 2021 na 2022 wanafunzi 1,369 walisajiliwa kufanya mitihani ya upimaji wa majaribio kwenye shule 23 za sekondari kidato cha nne zilizosajiliwa, lakini wanafunzi 106 walifeli na wanafunzi 2855 kidato cha pili walifanya mtihani wa upimaji 89 walifeli.
Saidi Magega mzazi amesema wanajua umuhimu wa elimu lakini changamoto walikuwa nayo ni hali ngumu ya maisha kwani wanashindwa kupata mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni.
""Sio kama hatutaki kupeleka wanafunzi wakasome ila hali ngumu hakuna hela ya kununua sare," amesema Magega.
0 Comments