Ajali hiyo ilitokea usiku wa Aprili 9 mwaka huu ambapo, Njovu, mkazi wa Lizabon Manispaa ya Songea akiendesha gari hilo aina ya ya Mitsubishi Fuso lilitumbukia mtoni.
Mara baada ya ajali hiyo, Njovu alitoweka kusikojulikana na jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya aliliambia gazeti hili kuwa wamemkamata.
“Leo (jana) saa nne asubuhi katika stendi ya Super Feo iliyopo Mahenge tumemkamata akijiandaa kutoroka na kwa kuwa tulishasema jeshi la polisi lina mkono mrefu ndivyo ilivyotokea,” alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani Jumatatu kwa hatua zaidi za kisheria.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kufuata sheria za usalama barabarani na madereva kuzingatia sheria kuepusha ajali zinazoweza kuepukika, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za waharifu ili mkoa uendelee kuwa salama.
0 Comments